CCM: Hatuhusiki na CHADEMA kuzuiwa kufanya shughuli zake

0
40

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakihusiki kwa namna yoyote na kufungiwa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya shughuli zake.

Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia Katibu Mwenezi CCM, Kenani Kihongosi ni kufuatia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku Januari 19, 2026 wakati akizungumza na vyombo vya Habari ambapo alihoji uhalali wa CCM kufanya kazi zake wakati CHADEMA kikiwa kimefungiwa.

CCM imefafanua kuwa kuzuiwa kwa CHADEMA kunatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu kufuatia migogoro ya ndani ya chama hicho, ambapo wanachama watatu wakiongozwa na Said Issa waliwasilisha maombi dhidi ya wadhamini na Katibu mkuu wa CHADEMA kuwa Mahakama izuie shughuli za chama.

CCM imeshauri Watanzania na watu wote wenye nia njema na Tanzania kupuuza taarifa hizo, pamoja na kujiepusha na kauli zozote za chuki zinazokusudia kuyumbisha Taifa.

Send this to a friend