CCM: Vyama vya upinzani viwe huru kususia uchaguzi

0
15

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamidu Shaka amevitaka baadhi ya vyama vya upinzani kuwa huru kususia uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa ni haki yao na hata vikifika maamuzi hayo chama hicho hakitayumba kwa kuwa kimejipanga kuchukua tena dola mwaka 2025.

Ameyasema hayo Unguja wakati akihutubia wananchi waliojitokeza kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambapo amesema kuwa mapokezi makubwa aliyoyapata Rais Dkt. Mwinyi ni ishara ya wazi kuwa wananchi wameridhishwa na uongozi wake.

Rais Dkt. Samia Suluhu atunukiwa tuzo ya kimataifa nchini India

“Nimekuwa nikisikiasikia wameanza kusemasema kwamba wanafikiria sijui tutasusa, sasa sijui msuse msisuse shughuli ipo kitu hiki hapa. Niwaombe wana-CCM wenzangu msipoteze muda wa malumbano na majibizano, tuna kazi ya kujenga chama, tuna kazi ya kujenga nchi hii,” amesema.

Ameongeza kuwa kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama hicho ni ‘kutesti mitambo’ tu na kwamba muda ukifika wapinzani wataupata ujumbe, hivyo wakae kwa kutulia kwa kuwa hakuna mjadala katika hilo na wala hakuna kubembelezana.

Send this to a friend