CCM yakemea bendera yake kutumika kufanya uhalifu

0
52

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara kimelaani kitendo cha watuhumiwa wa usafirishaji wahamiaji haramu kutumia bendera ya chama hicho kufanyia uhalifu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM mkoani humo, John Nzwalile medai watuhumiwa wametumia bendera ya CCM kwenye gari ili kufanya uhalifu na kukichafua chama hicho, jambo ambalo haliwezekani hata kama lingekuwa gari la chama hicho.

“CCM ni chama makini kinachojali uadilifu, hivyo vyombo husika vichukue hatua kali kwa wote waliohusika katika tukio hilo la kutumia bendera yetu na kufanya uhalifu,” amesema Nzwalile.

Ndugu wajiua baada ya baba yao kumpa shamba mke wake wa zamani

Aidha, Jeshi la Polisi mkoani humo lilieleza kuwa linamshikilia Edward Erihard (31), mkazi wa Dodoma kwa tuhuma za kusafirisha wahamiaji haramu 20 raia wa Ethiopia aliowabeba kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser huku gari hilo likiwa linapeperusha bendera ya CCM ili kuonesha kuwa kiongozi wa chama hicho anasafiri.

Send this to a friend