CCM yapitisha pendekezo la bima ya afya kwa watu wote

0
36

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) leo Juni 23, 2022 wamepitisha mapendekezo ya bima ya afya kwa wote nchini katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Afya ya kuimarisha mfumo wa bima ya afya iliyofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hatua hiyo inapelekea Wizara ya Afya kwenda kutunga sheria ya bima ya afya kwa wote na kuongeza kuwa kiasi kitakacholipwa na mwananchi kwa mwaka kitampa huduma za matibabu kama mtumishi wa Serikali, kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya, hospitali ya Wilaya, Rufaa za Mkoa, Kanda, Maalumu na hata Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Hii itasaidia kwa Watanzania wote kupata huduma bora za afya bila kikwazo cha fedha. Pia, Serikali itahakikisha dawa zinapatikana kwa wakati na zinazokidhi mahitaji ya wagonjwa,” amesema Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa na bima ya afya kwa wote ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 ya kuimarisha mfumo wa bima ya afya nchini ikiwemo mifuko ya bima za afya (NHIF na CHF) ili kufikia lengo la Serikali la kuwa na bima ya afya kwa wananchi wote.

Send this to a friend