CCM yashinda ubunge Moshi Mjini kwa mara ya kwanza tangu 1995

0
20

Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kushinda nafasi ya ubunge katika Jimbo la Moshi Mjinj kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 25 ya chaguzi za mfumo wa vyama vingi Tanzania.

Kufuatia matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi kwenye jimbo hilo, mgombea wa CCM, Priscus Tarimo ameibuka mshindi katika uchaguzi wa 2020 baada baada ya kupata kura 31,169 akifuatiwa na Raymond Mboya (CHADEMA) aliyepata kura 22,555.

Katika uchaguzi wa mwaka 1995, upinzani ishinda majimbo sita kati ya majimbo tisa mkoani Kilimanjaro ambayo ni Hai, Siha, Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Vunjo, na Rombo huku CCM ikishinda majimbo ya Mwanga, Same Mashariki na Same Magharibi.

Lakini katika chaguzi za mwaka 2000 na 2010, CCM ilifanikiwa kushinda katika majimbo ya Siha na Moshi Vijijini lakini mwaka 2015 majimbo hayo yalirudi mikononi mwa upinzani.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020, matokeo ambayo tayari yameshatolewa na NEC yanaonesha kuwa CCM imefanikiwa kushinda katika majimbo ya Hai na Moshi Mjini, lakini bado matokeo katika majimbo mengine hayajatangazwa.

Katika hatua nyingine, CCM imefanikiwa kushinda ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini ambalo kwa miaka 10 limekuwa likishikiliwa na mbunge wa CHADEMA.

Send this to a friend