CCM yatangaza sifa za wanaotakiwa kuwa Spika, Naibu spika na Meya

0
42

Baada ya kuamilika kwa uchaguzi kuu, Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimeoata ushindi mkubwa kimewaalika wananchama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za vyombo vya uongozi ikiwa ni pamoja na nafasi ya Spika na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema nafasi nyingine ambazo wanachama wanaweza kuomba ni pamoja na meya wa halmashauri ya jiji au manispaa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya.

“Msisitizo unawekwa kwamba sambamba na sifa stahiki kwa mujibu wa Sheria za nchi, waombaji wote lazima wawe wamekidhi sifa za uongozi,” imeeleza taarifa hiyo.

Tarehe ya kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi zote tajwa ni leo Novemba 2, 2020 na Novemba 3, 2020.

Chama hicho kimejipambanua kuwa kinaanza kazi mara moja kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo, hivyo kitahakikisha safu za uongozi zinakamilika kwa haraka.

Send this to a friend