CCM yawapa wiki moja mawaziri wa Elimu na TAMISEMI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa wiki moja kuanzia leo Januari 20, 2023 kwa Wizara ya Elimu na TAMISEMI kuhakikisha vishikwambi vilivyotolewa na serikali kwa ajili ya walimu vinawafikia walengwa.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Edward Mjema amesema CCM imepokea malalamiko ya kutotekelezwa kikamilifu kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu ugawaji wa vishikwambi hivyo.
Familia ya Mtanzania aliyeuawa vitani Ukraine imesema ilimzuia asiende vitani
“Ulitengwa muda maalumu wa kutolewa kwa vishikwambi hivyo ambao ulikuwa unaishia Januari 15, mwaka huu, lakini chama kimepokea malalamiko kwamba hadi leo kuna baadhi ya makundi hayajapata hivyo vishikwambi. Lakini pia kuna baadhi ya wilaya hawajagawa kabisa vishikwambi hivyo,” amesema.
Ameongeza, “kuna maeneo mengine unakuta walimu wako 10 na wote wanahitaji na wanastahili kupata, lakini unakuta vishikwambi vinatoka vinane, wawili wanaachwa.