CCM Zanzibar yapendekeza Dkt. Mwinyi kuongoza kwa miaka saba

0
45

Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wamepitisha pendekezo la kuishauri Kamati Maalumu kuridhia kuongeza muda wa Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi kuongoza nchi katika muhula wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka saba badala ya mitano.

Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Dimwa amesema uamuzi huo umetokana na kuridhishwa na kasi yake ya kiutendaji katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa zaidi ya asilimia 100 ndani ya kipindi miaka mitatu.

“Wajumbe wa sektetarieti tumejadili na kutathimini kwa kina juu ya utendaji wa Rais Mwinyi, tukajiridhisha hakuna mbadala wake na anastahiki aongoze nchi kwa kipindi cha miaka saba ili apate muda mzuri wa kufanya Mapinduzi ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi na kijamii,” amesema Dkt. Dimwa.

Ameongeza kuwa CCM Zanzibar imeona Serikali kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa kuwa ni wananchi wanahitaji maendeleo endelevu

Send this to a friend