CEO NMB ashiriki mkutano wa Benki ya Dunia, akutana na Rais wa taasisi hiyo

0
55

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna ameshiriki uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review) unaofanyika kwa siku tatu Zanzibar.

Huu ni Mkutano wa 20, lengo likiwa ni kufanya tathmini ya Muda wa Kati kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Benki ya Dunia.

Mkutano huo umefunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi na kuhudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar – Hemed Suleiman Abdalla, Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Mhe. Mwigulu Nchemba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania – Emmanuel Tutuba na viongozi wengine.

Akiwa katika mkutano huo, Bi. Ruth alipata nafasi pia ya kukutana na Rais wa Benki ya Dunia – Ajaypal Singh Banga.

Benki ya NMB inajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha mkutano huu mkubwa Tanzania unao wakutanisha wajumbe zaidi ya 3,000 kutoka mataifa takribani 100 duniani.

Send this to a friend