Cesar Manzoki atimkia China

0
48

Klabu ya Vipers Sports Club imethibitisha kuwa mshambuliaji wake, Cesar Manzoki amekamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Dalian Pro FC inayoshiriki Ligi Kuu ya China.

Mshambuliaji huyo mahiri, alijiunga na Venoms mwanzoni mwa kampeni ya 2020/21 na akaendelea kufanya vizuri kama mshambuliaji muhimu kwenye kikosi na pia kipenzi cha mashabiki.

Cesar licha ya kukabiliwa na majeraha kadhaa msimu wa kwanza, alicheza mechi 27 katika mashindano yote na kumaliza akiwa na mabao 14.

Aliweza kufunga mabao saba kwenye Ligi Kuu ya Uganda (SUPL), na aliongeza mabao saba katika Kombe la Stanbic Uganda 2021, kombe ambalo alishinda kama mfungaji bora wa mashindano hayo na kutwaa Kiatu cha Dhahabu.

Kwa ujumla, mshambuliaji huyo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) alicheza michezo 56, alifunga mabao 32 na alitoa usaidizi wa magoli 15, hivyo kumfanya kuhusika katika magoli 47.

Kabla ya kujiunga na Vipers, Manzoki alikuwa AS Vita (DRC) ambako alifunga mara 34 na kuongeza pasi za mabao 18 katika misimu miwili ya 2018 na 2019.

“Wapenzi Venoms, ni ngumu kwangu kupata maneno sahihi ya kusema kwaheri. Nitafurahia milele nyakati nzuri na mafanikio katika miaka yangu miwili,” ulisomeka ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii

Send this to a friend