CHADEMA: Hatujasema hatutashiriki uchaguzi 2025

0
40

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema katika uchaguzi wa mwaka 2025 si kwamba hawatoshiriki uchaguzi bali uchaguzi huo hautafanyika ikiwa tume huru ya uchaguzi haitopatikana.

Akizungumza Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje CHADEMA, John Mrema amesema bila ya kuwepo kwa tume hiyo ni kupotezeana wakati hivyo wakati sahihi utakapofika chama hicho kitatangaza utaratibu utakaotumika.

“Msimamo wetu na huwa tunahesabu sana maneno. Hatujawahi kusema hatutashiriki, tumesema uchaguzi hautafanyika,” amesema.

Tanzania yatajwa kuwa nchi yenye mafanikio ya demokrasia na utawala bora

Ameongeza “Mpaka sasa msimamo wetu ni kwamba ni lazima Serikali ijue uchaguzi unaosimamiwa na tume hii jinsi ilivyo na muundo wake, huu uchaguzi CHADEMA hatuoni kama ni busara kwenda kushiriki.

Aidha, amesema CHADEMA imewahi kuipeleka Serikali katika Mahakama ya Haki ya Afrika kupinga tume ya uchaguzi na kushinda kesi hiyo lakini Serikali haitaki kufuata maagizo ya mahakama hiyo.

Send this to a friend