CHADEMA na ACT Wazalendo wapinga matokeo, wataka uchaguzi wa marudio

0
47

Vyama vya upinzani Tanzania, ACT-Wazalendo na CHADEMA vimesema haviyatambui matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Katika mkutano wa pamoja uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, vyama hivyo vimetoa tamko lenye matakwa kadhaa ambayo ni kufanyika kwa uchaguzi wa marudio pamoja na kuundwa kwa Tume Huru itakayosimamia uchaguzi huo wa marudio.

Aidha, vyama hivyo vimelaani vurugu zilizoibuka maeneo balimbali nchini kipindi chote cha uchaguzi na kupelekea baadhi ya wananchi kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.

Pia, chama hicho kimeitisha maandamano ya amani nchini kote kuanzia Novemba 2, 2020 ikiwa ni kushinikiza kutekelezwa kwa matakwa yako, na kueleza kuwa hawatokoma kuendelea kudai haki ya uchaguzi huru.

Tamko la vyama hivyo limekuja saa kadhaa baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa ndiye mshindi wa kinyag’anyiro hicho.

Dkt. John Magufuli aliibuka mshindi baada ya kupata kura 12,516,252 sawa asilimia 84.4 ya kura zote halali 14,83195.

Mshindani wake kupitia chama kikuu cha upinzani, Tundu Lissu (CHADEMA) amepata kura 1,933,271 sawa na asilimia 13.04.

Send this to a friend