CHADEMA: Tunamtambua Mbatia kama Mwenyekiti NCCR-Mageuzi

1
39

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika ameiomba mamlaka zinazohusika kusimamia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuchunguza utendaji kazi wa Msajili na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa.

Ameyasema hayo leo katika mkutano na vyombo vya habari jijini Dar es salaam ambapo amedai ofisi ya msajili imekuwa ikipandikiza migogoro katika vyama na kubadilisha ‘kiharamu’ uongozi ndani ya vyama vya siasa.

Aidha, Mnyika ameeleza kuwa CHADEMA inamtambua James Mbatia kama Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi licha ya kusimamishwa na halmashauri kuu ya chama hicho.

“Kwa upande wetu sisi CHADEMA mpaka katika hatua ya sasa, tunamtambua kwamba James Mbatia ndiye Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na tunatoa mito kwa wadau wote kumulika matendo ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo kimsingi yanavuruga utulivu katika vyama,” amesema.

NCCR Mageuzi yamsimamisha Mbatia

Hata hivyo, Mnyika ameomba vyama vya siasa ambavyo ni wadau muhimu katika kuitafuta haki, demokrasia na siasa visiingiliwe kwa njia haramu na visitengenezewe migogoro haramu.

Send this to a friend