CHADEMA: Uandaaji wa kanuni za mikutano ya hadhara ni uhuni

1
89

Kikao kilichojumuisha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Baraza la vyama vya siasa pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, cha kujadili kanuni maalum za kuratibu mikutano ya hadhara, kimeleta matumaini ya kurejea kwa mikutano hiyo iliyozuiliwa nchini.

Aidha, kikao hicho kimehudhuriwa na vyama 18 vya siasa isipokuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wamedai kuwa uandaaji wa kanuni hizo ni ‘uhuni’ unaotaka kupora uhuru wa mikutano hiyo.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema Rais Samia Suluhu Hassan alimuelekeza waziri mwenye dhamana ya siasa na ofisi ya waziri kwamba zitungwe kanuni za kuratibu mikutano ya hadhara ili ifanyike kwa amani bila kuzuia shughuli za maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo amesema miongoni mwa mambo mengine waliyokubaliana katika kanuni hizo ni kuepuka lugha za matusi, badala yake wajadili hoja za msingi.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lyimo ameongeza kuwa Jeshi la Polisi lina mamlaka ya kuamua uhalali wa mikutano hiyo na kushauri lipewe taarifa tu na si vinginevyo.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend