CHADEMA yaeleza sababu za kutosaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi

0
3

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema maamuzi ya kutosaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi mwaka 2025 ni kutokana na kutokuwepo kwa majibu ya maadishi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu barua rasmi iliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Desemba 29, 2024.

Taarifa iliyotolewa na CHADEMA imesema barua hiyo ilieleza mapendekezo na madai ya msingi kuhusu mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

“Ukimya huu unathibitisha kukosekana kwa nia ya dhati ya kufanya mashariano ya kweli na ya wazi kuhusu mchakato wa uchaguzi,” imesema taarifa hiyo.

Imeongeza kuwa “CHADEMA ilishapitisha maamuzi yanayojulikana kama ‘Bila Mabadiliko Hakuna Uchaguzi’ ambayo yanasimamia hitaji la kufanyika kwa mageuzi ya msingi ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.”