CHADEMA yaitaka serikali itaje hadharani makosa ya Tanzania Daima

0
23

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kusikitishwa na uamuzi wa serikali wa kufuta leseni ya uchapishaji na usambazaji wa Gazeti la Tanzania Daima kuanzia leo Juni 24, 2020, kitendo ambacho chama hicho kimesema kinakiuka haki ya umma kupata taarifa.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene, chama hicho kimeeleza mambo mablimbali ikiwa ni pamoja na kuitaka serikali kuueleza umma wa Watanzania makosa yaliyofanywa na gazetu hilo na kupelekea kukiuka Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya Mwaka 2016.

Aidha, CHADEMA kimeitaka serikali kueleza kililionya gazeti hilo mara 10 katika masuala gani, serikali itaje habari ambazo zilikosewa na kupelekea gazeti tajwa kuonywa, ilipatie gazeti hilo haki ya kusikilizwa dhidi ya uamuzi huo na kurejesha leseni ya kuchapisha na kusambaza gazeti.

Taarifa hiyo ya CHADEMA imekuja ikiwa ni siku moja tangu serikali ilipotangaza uamuzi wa kusitisha leseni ya Gazeti la Tanzania Daima kutokana kukiuka sheria pamoja na maadili ya uandishi wa habari.

Send this to a friend