CHADEMA yataja ajenda zake kuu tatu kuelekea 2025

0
34

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, chama kimeandaa mkakati katika ajenda tatu ambazo ni mapambano, mazungumzo na maandalizi kwa kuwa safari ya ukombozi sio nyepesi.

Ameyasema hayo katika kikao cha baraza la uongozi la kanda ya Victoria lililofanyika jana mjini Geita na kueleza kuwa mlango wa mazungumzo umefunguliwa na kuwasihi wanachama wasibwete.

“Pamoja na kuwepo na mazungumzo na mapambano ya kudai katiba, haki za siasa na za wananchi, lazima tufanye na la tatu ambalo ni kuanza sasa maandalizi ya uchaguzi wa 2025,” amesema.

Aidha, amebainisha kuwa, kitendo cha Chama cha Mapinduzi kukubali kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya, kimempa matumaini licha ya kuwa ni maamuzi yao, lakini ni matokeo ya msimamo wa CHADEMA na wengine wa kutaka katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi wa 2025.

Amesema, kinachotakiwa ni kufanya mazungumzo ili katiba itakayopatikana iwe bora na pia iwe na muundo mpya utakaowakilisha maslahi ya wananchi na kujenga muafaka wa Kitaifa na siyo wa chama kimoja.

Send this to a friend