CHADEMA yatakiwa kujieleza kwa Msajili sababu ya viongozi waliomaliza muda kuendelea kukaa madarakani

0
11

Msajili wa Vyama vya Siasa amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukitaka kijieleze haraka kwa nini kisichukuliwe hatua za kisheria kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa, katiba na kanuni za chama hicho kwa kutofanya uchaguzi wa viongozi.

Msajili amefikia hatua hiyo baada ya viongozi Wakuu wa CHADEMA kuendelea kuwa viongozi wakati uongozi wao ulifikia mwisho tarehe 14 Septemba 2019 kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA Ibara ya 6.6.3 inayochagizwa na Ibara ya 6.3.2(a) inayosema kila kiongozi wa CHADEMA atakaa madarakani kwa muda wa miaka 5.

Msajili amekitaka CHADEMA kitoe sababu kwanini kisichukulie hatua kali kwa mujibu wa kifungu cha 4(5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258.

Send this to a friend