CHADEMA yatangaza kutoshiriki uchaguzi wa madiwani

0
46

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakitashiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye Kata 14 zilizopo katika Halmashauri 13 nchini ambazo zimetangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

CHADEMA imesema uchaguzi huo utasimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, jambo ambalo ni kinyume na uamuzi wa mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Haki za Watu katika uamuzi wake uliotolewa Juni 13, 2023 baina ya Chacha Wangwe dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“CHADEMA tunatangaza kuwa hatutashiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Tunataka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Afrika na kutekeleza uamuzi uo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wowote nchini,” imesema CHADEMA.

Aidha, imeitaka Serikali kuharakisha mchakato wa kupata Katiba Mpya ambayo itakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na mabadiliko mengine ambayo yataweza kusimamia uchaguzi ulio huru na haki.

Send this to a friend