CHADEMA yatangaza tarehe ya kuanza kwa mikutano ya hadhara

0
50

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imetangaza Januari 21 kuwa siku ya uzinduzi wa mikutano ya hadhara kitaifa.

Taarifa ya kamati imeeleza kuwa baada ya uzinduzi huo utafuatiwa na uzinduzi wa mikutano ya hadhara kwenye kila makao makuu ya Kanda na baadaye ngazi nyingine za chama zitaendelea na mikutano kwenye ngazi zao.

Maazimio hayo ni kufuatia kikao cha dharura cha kamati kuu ya chama kilichoketi Januari 5, 2023 kujadili taarifa ya mwenendo wa mazungumzo ya maridhiano baina ya timu ya CHADEMA inayoongozwa na Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe na Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Abdulrahman Kinana.

Aidha, kamati kuu imesema imeridhishwa na mwenendo wa mazungumzo hayo pamoja na hatua ambazo zimechukuliwa mpaka sasa na kuitaka timu ya mazungumzo iendelee na mazungumzo ya maridhiano hayo.

Send this to a friend