CHADEMA yatishia kutoshiriki uchaguzi mkuu 2025

0
44

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimegoma kushiriki chaguzi ndogo zitakazofanyika Desemba 17, mwaka huu huku ikitishia kususia uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu 2025 endapo hakutakuwa na mabadiliko ya katiba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Novemba 22, 2022 katika makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Bara, Singo Kigaila amesema msimamo wa chama hicho ni kutoshiriki chaguzi zote ndogo kipindi hiki.

“Tumepokea taarifa ya tume kuwa na uchaguzi wa jimbo la Amani, Zanzibar na kata 12 za Halmashauri mbalimbali za bara, kama chama msimamo wetu huko pale pale hatutoshiriki.

“Kwenye chaguzi hizi, msimamo wa chama ni kwamba hatushiriki, hatuwezi kushiriki kwenye ‘maigizo’,” amesisitiza.

Kuhusu uchaguzi wa mwaka 2024 na 2025, amesema wako kwenye majadiliano na Serikali ya kutaka uwepo wa katiba mpya ambayo itazaa tume huru ya uchaguzi, sheria na muundo bora wa uchaguzi.

Send this to a friend