Chalamila atoa wiki mbili mabasi 70 ya Mwendokasi yarekebishwe

0
46

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa wiki mbili kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuhakikisha mabasi 70 mabovu yanafanyiwa marekebisho na yarudi kuendelea na kazi ili kuondoa kero ya usafiri huo kwa wananchi waishio mkoani humo.

Akizungumza wakati aliopotembelea kituo cha mabasi ya mwendokasi Kimara, Dar es Salaam amesema anashangazwa kwanini idadi kubwa ya mabasi hayo ni mabovu licha ya kuwa mtoa huduma analipwa fedha katika mradi huo, jambo linalopelekea ongezeko la mahitaji kwa wananchi.

Ujenzi Mwendokasi Posta- Boko kuanza Oktoba 15

“Sitakuwa tayari kuona Rais Samia Suluhu Hassan aliye na nia njema na huu mradi anatukanwa kwa sababu tu ya uzembe wa watu fulani kushindwa kutimiza majukumu yao,” amesema Chalamila.

Kwa upande wa DART katika mahojiano na gazeti la Mwananchi Oktoba 11 mwaka huu ulisema kufurika kwa abiria hususani wa kituo cha Kimara kunasababishwa na watu wengi asubuhi kuelekea upande mmoja, pia kutokuwa na mfumo rasmi wa kuongozea mabasi hayo.

Send this to a friend