Chalamila: Marufuku kulazimisha wafanyabiashara kufunga maduka ili kufanya usafi

0
37

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amewapiga marufuku watumishi wa kata na mitaa kuwalazimisha wafanyabiashara kufunga maduka yao ili kufanya usafi.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 23, 2022 wakati akizungumza na Shirikisho la Umoja wa Wamachinga, Mama Lishe/Baba Lishe, Jamii Mpya, Wanawake Wafanyabiashara, Jukwaa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi na Shujaa wa Maendeleo wa Mkoa wa Kagera, ikiwa ni mwendelezo wa kuzungumza na makundi mbalimbali ya kijamii.

Chalamila ameongeza kuwa “dhana hii ya kuchagua siku moja kuwa ni siku ya usafi inarudisha nyuma ukuaji wa kiuchumi na kupelekea baadhi ya wafanyabiashara kutofungua biashara zao.”

Aidha, amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa zilizopo kwa kuwa wasipoifanya hivyo watakuja wageni na kukimbilia fursa hizo na wazawa kubaki bila maendeleo.

Send this to a friend