Chalamila: Uchunguzi umebaini moto Kariakoo ni hujuma za wafanyabiashara

0
49

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kamati aliyoiundwa kuchunguza chanzo cha moto eneo la Mnadani, Kariakoo imebaini moto huo haikuwa ajali bali ilikuwa ni hujuma kutoka kwa wafanyabiashara wenyewe.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kamati hiyo ilipewa jukumu la siku saba kuhakikisha wanakamilisha angalau hatua za awali za uchunguzi wa chanzo cha moto huo, huku ukihusisha ukaguzi wa eneo la tukio, pamoja na mahojiano ya kina na wamiliki pamoja na mashuhuda mbalimbali.

“Kamati imebaini kwamba moto huo haukuwa ajali bali ilikuwa ni hujuma ndani ya wafanyabiashara wenyewe, na moto huo ulianzaia katika eneo la Mnadani, Kariakoo. Maelezo yote haya yalibainika katika baadhi ya kamera za CCTV ambazo zilikuwa pembezoni wakati moto unaanza taratibu kabla haujaingia kwenye majengo mengine,” ameeleza.

Biashara 5 ambazo hupaswi kufanya ukiwa na mtaji mdogo

Aidha, amesema uchunguzi huo umebaini kuwa jenereta ambalo awali wafanyabiashara walidai ndio chanzo cha moto huo, ni zima na wala halikuwa chanzo cha moto huo.

Chalamila amesema kamati imeshauri Serikali iwatafutie wafanyabaisahara wa soko hilo eneo mbadala ili kuepusha athari kubwa pindi kunapotokea majanga ya moto kutokana na biashara hizo kuwa katikati ya majengo.

Halikadhalika, amevielekeza vyombo vya dola kuchukua hatua za kiuchunguzi na kuwabaini wote waliohusika kutekeleza tukio hilo, ili hatua za kisheria ziweze kufuatwa.

Send this to a friend