Chalamila: Walioziba vichochoro Kariakoo wabomoe kwa mikono yao 

0
32

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mpaka sasa bado haijabainika chanzo cha moto uliozuka eneo la Kariakoo huku akiwataka walioziba vichochoro kuzibua haraka iwezekanvyo ili kutoa urahisi pindi majanga yanapotokea.

Akizungumza eneo la tukio, amesema moto ulianza kwenye jengo moja kisha kutapakaa zaidi lakini mpaka sasa hakuna taarifa za vifo vyovyote vilivyokana na moto huo.

“Wale wote walioziba vipenyo ambavyo tunaingia kwa mujibu wa ramani, wao wenyewe wachukue hatua kubomoa vipenyo hivyo ili tuendelee kujidhatiti kama kukitokea majanga mengine kama hayo. [..] ukiangalia hakuna vichochoro vya kuelekea huko tunakokwenda, sasa waanze kubomoa kwa mikono yao wenyewe,” amesema.

Aidha, amelishukuru Jeshi laa Zimamoto na Uokoaji kwa juhudi kubwa walizofanya katika kudhibiti moto huo huku akiwaasa wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya moto yanayoweza kusababisha athari.

Send this to a friend