Chama cha Wanasheria Tanganyika chaahidi ushirikiano kwa serikali

0
48

Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambapo Rais wa chama hicho, Profesa Edward Hoseah amesema wameomba kukutana na Rais ili kujitambulisha na kuelezea  majukumu yao. 

Profesa Hoseah amesema pamoja na mambo mengine, TLS ina jukumu la kumshauri Rais, serikali, bunge na mahakama katika masuala mbalimbali ya sheria na utawala bora. 

Aidha, Profesa Hoseah amemhakikishia Rais Samia kuwa TLS iko tayari kuendelea kushirikiana na kuishauri  Serikali katika masuala mbalimbali ya kisheria.

Kwa upande wake Rais Samia ameishukuru na kuipongeza TLS kwa kazi nzuri inayofanya katika kutekeleza majukumu yake  ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali. 

Rais ameihakikishia TLS ushirikiano wa kufanya nao kazi kwa karibu ili kuweza kutimiza majukumu yake pia amepokea changamoto zao mbalimbali. 

Send this to a friend