Chama cha wasioona Tanzania waneemeka na msaada kutoka Meridianbet

0
58

Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) kwa furaha kubwa wamepokea msaada wa fimbo za kutembelea “White canes” kutoka Meridianbet Tanzania ikiwa ni moja ya utamaduni wa kampuni hiyo kuyashika mkono makundi yenye mahitaji maalum pamoja na jamii kwa ujumla kwa kutoa misaada mbalimbali.

 Akitoa ushuhuda wake akiwa haamini kile kilichotokea, Katibu wa Chama hicho ndugu Iddi Kiwimbi alisema kwamba Meridianbet wamefanya kitu kikubwa ambacho hakuna kampuni yeyote imewahi kufanya hivyo.

“Niwambie ndugu zangu hawa watu nimewafahamu siku ya Alhamisi walinipigia simu kuniambia kuna ujumbe wako kwenye Email tunataka kuja kutoa msaada, Nilishangaa sana, kwa sababu sisi ndio huwa tunatafuta sehemu ya kupata misaada ila wao wameguswa moja kwa moja na kututafuta” – Iddi Kiwimbi- Katibu wa Chama cha watu wenye ulemavu wa macho.

” Sisi tuseme nini tena zaidi ya kuwashukuru kwa sababu mmekumbuka kwamba kuna ndugu zetu wana changamoto mbalimbali, pamoja na mahitaji hayo ni fimbo kwa sababu mnajua umuhimu wake, kwakweli tunawashukuru sana sana” Iddi Kiwimbi.

Akitoa neno mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Meridianbet Tanzania Ndugu Matina Nkurlu alisema:

“Tumefika hapa kutoa msaada kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa macho, tuliguswa na tukaona kuwatembelea ili tuwape kile kidogo tunachokipata ikiwa ni utamaduni wetu Meridianbet Tanzania kila mwezi huwa tunatoa kwa jamii kidogo tunachokipata kama shukrani”- Matina Nkurlu

“Kama mnavyoona hali ya ofisi yao ni hali duni kabisa kwahiyo basi naomba nitumie fursa hii kuomba makampuni mbalimbali kuwakumbuka ndugu zetu sio tu kwa sababu wana matatizo ya macho tuwatenge hapana, huu ndio wakati na msimu wa Sikukuu tuwajali na wao wafurahie, basi naomba makampuni mengine yaige mfano wa Meridianbet Tanzania.” -Matina Nkurlu

Msaada huo wa vifaa vya kusaidia kuwaongoza wakati wa kutembea, ulitolewa na Meridianbet Tanzania kwa chama hicho maeneo ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam, ambapo utaenda kusaidia kundi hilo lenye uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo vyenye gharama kubwa hali inayopelekea baadhi yao kushindwa kumudu gharama hizo.

 

 Hii hapa nyingine usikubali ikupite, mwezi Disemba ni mwezi wa kufurahi, hivyo kuifanya siku yako iende poa, Meridianbet wanakuletea promosheni ya SAKA MBUZI NA KITOCHI, ukibeti bila bando kwa dau la kuanzia TZS 1,000/= Promosheni hii itadumu kwa mwezi huu wa Disemba tu. Piga *149*10# kubeti sasa.

 

Send this to a friend