Chama tawala Namibia chamchagua mgombea Urais mwanamke

0
37

Chama tawala nchini Namibia kimemchagua Netumbo Nandi-Ndaitwah kuwa Makamu wa Rais wa chama hicho, na hivyo kumweka katika mstari wa kuwa mgombea urais wa kwanza mwanamke wakati kiongozi huyo wa sasa atakapong’atuka Machi 2024.

Wakati wa mkutano wa chama hicho wanachama wa Chama cha Swapo walimchagua tena Netumbo-Nandi Ndaitwah, Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo, kama Makamu wake wa Rais.

Wanaume walalamika wake zao kutowashirikisha fedha wanazopata kwenye VICOBA

Kulingana na katiba ya Swapo, atakuwa mgombea urais wa chama wakati Rais aliyeko madarakani, Hage Geingob, atakapomaliza muda wake wa mihula miliwi miezi 15 ijayo.

Ndaitwah alipata ushindi rahisi katika duru ya kwanza dhidi ya wagombea wengine wawili, akiwemo bosi wake, Waziri Mkuu wa sasa.

“Jambo ninalojaribu kusisitiza ni kwamba hakuna wakati rahisi maishani. Kwa hiyo, kila wakati una changamoto zake na naweza kukwambia, vyovyote itakavyokuwa, kuna watu ambao wako tayari kukabiliana na changamoto hizo na mimi ni mmoja wapo. Huu ndio wakati niliopewa ili kushika nafasi hiyo. Nawaomba wanachama wa chama wanipe nafasi hiyo na niko tayari,” amesema.

Chama hicho kimeiongoza Namibia tangu mwaka 1990 huku kikiungwa mkono na wananchi wengine, jambo ambalo linatoa fursa kwa mwanamama huyo kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo.

Send this to a friend