Chaneli 15 za YouTube zinazoongoza kwa kutazwa Tanzania

0
56

Mtandao wa YouTube si tu umekuwa sehemu ya watu kujiburudisha na kupata ujuzi kuhusu mambo mbalimbali, bali pia umekuwa chanzo cha fedha kwa watu wengi.

Kiasi cha fedha utakachoingiza kinategemeana sana na utazamwaji wa video zako kwenye mtandao huo. Video zako au maudhui mengine yanavyotazwa kwa idadi kubwa ndivyo inakuwa kwenye nafasi ya kupata fedha zaidi.

Kutokana na hilo, wasanii, vyombo vya habari na watu wengine wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kukuza ushawishi wao kwenye mtandao huo, na leo tutazitazama chaneli 15 za YouTube kubwa zaidi nchini Tanzania.

Orodha hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Social Blade kwa kutazama idadi ya kutazwa mwa maudhui ya chaneli husika;

1. Diamond Platnumz – 1,665,769,709
2. Millard Ayo – 1,418,005,282
3. Global TV Online – 1,122,433,417
4. Rayvanny – 694,793,379
5. Harmonize – 683,915,867
6. Wasafi Media – 604,989,177
7. Azam TV – 461,735,295
8. Young Tubers – 402,403,620
9. Mbosso – 412,568,635
10. Li Dancer Chris – 297,691,717
11. Zuchu – 275,493,429
12. Alikiba – 194,106,472
13. Steve Mweusi – 181,118,994
14. Lava Lava – 179,449,218
15. Aslay – 166,629,576

Send this to a friend