Chanjo ya UVIKO19, RC Homera asitisha likizo za madaktari

0
48

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Home amesitisha likizo za waganga wakuu wa wilaya ili warejee kazini kuongeza nguvu ya kuhamasisha kampeni utoaji Chanjo ya UVIKO19 ya nyumba kwa nyumba.

Akizungumza kwenye ya semina ya kamati ya afya mkoani humo amesema zoezi la utoaji chanjo limekuwa likususua kutokana waganga wakuu kutoendesha vyema kampeni hiyo, ndio sababu ya kusitisha likizo, na warejee haraka kwenye vituo vya kazi.

Homera amesema watalaamu wa afya watapita nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda shuka kwa shuka kutoa chanjo hiyo, lakini akihimiza kwamba iwe hiari.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alizindua rasmi kampeni ya taifa ya chanjo ya Covid-19 Julai 28 mwaka huu na kuwa wa kwanza kuchanjwa akinuwia kuuhakikishia umma kuwa chanjo hiyo ni salama.

Send this to a friend