Chanzo cha ugonjwa wa presha ya macho na dalili zake

0
63

Ugonjwa wa shinikizo la macho au presha ya macho (Glaukoma) ni ugonjwa ambao huandamana na kuharibika kwa mshipa wa neva ya optiki (Optic nerve).

Ugonjwa huu mara nyingi hujitokeza kwa watu wa makamo hasa baada watu hao kutimiza au kuvuka miaka arobaini (40).

Kwa kiasi fulani unaweza kujitokeza zaidi kwa watu wenye vinasaba vinavyofanana, kwa hiyo wakati mwingine ugonjwa huu huonekana kwenye familia au ukoo fulani zaidi kuliko watu wengine.

Chanzo cha ugonjwa
•Kasoro za kimaumbile katika sehemu ya jicho ambayo kazi yake kubwa ni kutoa maji ndani ya jicho ili kuweka sawa uwiano kati ya presha ndani ya jicho na uzalishaji wa maji ndani ya jicho.

•Magonjwa ya macho au matumizi ya vifaa vyenye mwanga mkali pamoja na vumbi lenye kemikali.

•Kuumia jicho kwa kupigwa na kitu au kumwagiwa kemikali.

• Baada ya upasuaji wa macho wa kutibu tatizo lingine la macho inaweza kuwa chanzo kingine cha tatizo la presha ya macho.

Watu walio katika hatari ya kuugua;
Kundi la watu wanaougua ugonjwa wa kisukari, wenye umri zaidi ya miaka 40, walioumia macho, wanaotumia dawa fulani kama ‘predinisolone’ ambazo huathiri macho, waliopata ajali na wale wasioona vizuri wanaweza kupata tatizo hilo.

Dalili za ugonjwa;
Mara nyingi ugonjwa huu dalili zake haziji moja kwa moja bali huja kwa kujificha sana bila mhusika kujua.

•Moja ya dalili ya maradhi haya ni mtu kushindwa kuona mbali na pembeni.

•Kuhisi jicho zito

•Kutokwa na machozi

• Mgonjwa kuwa na macho mekundu na kusikia maumivu makali ya macho.

•Kuona ukungu

Njia za kuzuia;
Huwezi kuzuia maradhi haya lakini unaweza kuzuia upofu kwa kuanza matibabu mapema na kufuatilia kwa umakini kama utakavyoelekezwa na daktari.

Unashauriwa iwapo utakuwa na dalili zinazofanana na ugonjwa huu, hauna budi kuwahi kwenye kituo au hospitali yoyote inayotoa huduma za macho ili uweze kuchunguzwa kwa kina na kupewa matibabu sahihi.

Send this to a friend