Cheti cha chanjo ya Corona huenda kikahitaji utakapohitaji kusafiri kwenda mataifa mbalimbali

0
41

Wakati chanjo ya virusi vya corona ikiendelea kutolewa katika nchi mbalimbali duniani, watu wanahamu ya kuona wakiweza tena kufanya mambo mbalimbali kama kusafiri, kwenda sinema, kwenye kumbi za burudani na maeneo mengine. Lakini ili kuweza kufanya haya, huenda kukawa na sharti au hitaji moja, uthibitisho kuwa umepata chanjo ya corona.

Kampuni na makundi ya kiteknolojia duniani yameanza kuandaa programu tumizi (Apps) au mifumo kwa ajili ya watu kuweka taarifa zao ikiwemo majibu ya vipimo vya #COVID-19, taarifa za chanjo, ambapo wataweza kupata cheti cha kidijitali watakachotakiwa kuonesha kwenda au kuingia sehemu mbalimbali.

Programu tumizi ya CommonPass iliyotengenezwa na shirika la The Commons Project la Geneva ni mfano mzuri ambapo kupitia hiyo mtumiaji atatakiwa kuweka majibu ya vipimo, uthibitisho wa kupata chanjo kutoka kwenye hospitali au wataalamu wa afya. Programu hiyo imeanza kutumiwa na mashirika mbalimbali ya ndege kama Cathay Pacific, JetBlue, Lufthansa, Swiss Airlines, United Airlines na Virgin Atlantic ambapo masafiri analazimika kukidhi vigezo vya kiafya kabla ya safari.

Kampuni ya teknolojia ya IBM nayo imetengeneza programu, Digital Healthy Pass ambayo inawaruhusu wenye kumbi mbalimbali na makampuni kuweka vigezo wanavyotaka kuzingatia kabla ya kuwahudumia wateja wao ikiwa ni pamoja na kupima #COVID-19, kupata chanjo na joto la mwili.

Hata hivyo baadhi ya changamoto zinatajwa kuukabili ubunifu huo ambapo ni pamoja na usiri na usalama wa taarifa za mtumiaji pamoja na uwezo wa chanjo mbalimbali zinazotolewa kukabiliana na virusi hivyo.

Kutokana na changamoto ya baadhi ya watu kutokuwa na simu janja (smartphones) kuweza kutumia prpgramu hizo, COVID-19 Credentials Initiative inaandaa utaratibu (smart card) ambao utawawezesha wasio na simu za aina hiyo nao waweze kupata vyeti hivyo.

Send this to a friend