China kufadhili Trilioni 2.5 kuboresha reli ya TAZARA

0
47

China kupitia Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya Kiraia (CCECC) inapanga kutumia Dola za Marekani bilioni moja [TZS trilioni 2.5] kurekebisha reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA).

Balozi wa China nchini Zambia aliwasilisha pendekezo kwa Waziri wa Uchukuzi wa Zambia kuwekeza katika ukarabati wa reli ya TAZARA kupitia ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi.

Reli hiyo ilijengwa na kufadhiliwa na China mwaka 1976 na kuwa kiungo kikuu cha usafirishaji kati ya Tanzania na Zambia, pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini imeharibika kutokana na uchakavu.

Mradi huo ni wa mtandao wa reli wenye urefu wa kilomita 1,860 ambapo ufadhili huo utatolewa na Benki ya Maendeleo ya China.

Kwa mujibu wa utabiri wa mamlaka inayosimamia miundombinu, mtandao huo unatarajiwa kubeba tani 450,000 za mizigo na abiria milioni 3.4.

Send this to a friend