China kuongeza uwekezaji Tanzania

0
58

Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 21, 2021 amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa China, Xi Jinping.

Katika mazungumnzo hayo Tanzania na China zimekubaliana kukuza ushirikiano katika nyanja za uchumi, utamaduni na ushirikiano wa Kimataifa.

China imeahidi kufungua zaidi soko lake kwa bidhaa za Tanzania pamoja na kuongeza uwekezaji hususan katika sekta ya viwanda.

Aidha, kupitia mazungumzo hayo China imeahidi kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Send this to a friend