China yabadili masharti ya visa kwa wasafiri wa Tanzania

0
54

Serikali ya China kupitia ubalozi wake nchini Tanzania imefungua utoaji wa visa za kuingia nchini China kwa Watanzania kuanzia Julai 11 mwaka huu.

Ubalozi huo umefanya mabadiliko ya masharti ya utoaji wa visa za kuingia nchini humo ikiwemo kujumuisha cheti cha chanjo ya UVIKO-19, pia kwa mwombaji kutoa uthibitisho wa ukaaji wa Tanzania kwa ambao ni wageni, na vithibitisho vinavyoonesha sehemu anakofanyia kazi, mwajiri wake na mahali anakoishi.

Dhamana kuondolewa kwenye makosa ya ubakaji na ulawiti

Katika hatua nyingine, Ubalozi wa Tanzania nchini China umetoa tahadhari kwa Watanzania wanaopanga kununua bidhaa kwenye kampuni zilizoko nchini humo kwa njia ya mtandaoni kuwa makini ili kuepuka kuibiwa.

Akitoa taarifa hiyo Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amewakumbusha Watanzania kufanya upekuzi wa kampuni hizo kabla ya kufanya manunuzi, na kuongeza kuwa ubalozi unatoa huduma ya kuzitambua kampuni hizo.

Send this to a friend