China yadai Marekani imerusha maputo kwenye anga lake bila ruhusa

0
25

China imedai puto za Marekani zimeruka juu ya anga lake bila ruhusa kwa zaidi ya mara 10 tangu mwanzoni mwa mwaka 2022.

Shutuma hizo za China zimezidisha mzozo kati yake na Marekani ulioanza mwishoni mwa juma lililopita baada ya jeshi la Marekani kudungua puto linalosemekana ni kijasusi la China, na kumfanya mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani, Antony Blinken kughairi safari ya kwenda Beijing ili kupunguza hali ya wasiwasi.

Beijing imelaani uamuzi wa Washington kudungua puto hilo lililopita kwenye anga ya nchi hiyo, na kudai kuwa kitendo hicho kinaweza kuhatarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Wakandarasi waliojenga majengo yaliyoporomoka Uturuku wakamatwa

“Tangu mwaka jana puto za Marekani zimepita zaidi ya safari 10 haramu katika anga ya China bila idhini ya idara husika za China,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin amesikika akisema katika mikutano ya mara kwa mara mjini Beijing wakati akijibu maswali.

Hata hivyo, Msemaji wa Usalama wa Taifa wa White House nchini Marekani, John Kirby  Utamekanusha shutuma za China akidai madai hayo hayana ukweli.

Send this to a friend