China yaifungia kampuni kubwa ya teknolojia ya Marekani

0
41

China imetangaza kuwa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni ya teknolojia ya Marekani, Micron Technology, ni hatari kwa usalama wa taifa hilo.

Mamlaka ya udhibiti wa anga ya mtandao nchini humo imesema kampuni hiyo ambayo ni mtengenezaji mkuu wa chipu za kuhifadhia taarifa (memory chips) nchini Marekani inahatarisha usalama wa mtandao nchini humo.

“Uchunguzi umegundua kuwa bidhaa za Micron ni tishio kwa usalama wa mtandao, zinahatarisha usalama wa mfumo muhimu wa usambazaji wa miundombinu ya habari ya China, na zinaweza kuathiri usalama wa kitaifa wa China,”Mamlaka ya usimamizi wa Mtandao wa China (CAC) imesema katika taarifa.

Mkuu wa jeshi la Sudan amfukuza kazi kamanda wa jeshi la akiba

Hatua hiyo inamaanisha chipu za kampuni hiyo zitapigwa marufuku kushiriki katika miradi muhimu ya miundombinu katika nchi hiyo ambayo uchumi wake ni wa pili kwa ukubwa duniani.

Serikali ya Marekani imepinga vikali madai hayo na kueleza kwamba itafanya kazi na washirika kushughulikia kile kilichoitwa ni upotoshaji wa soko la bidhaa hiyo unaosababishwa na China.

“Tunapinga vikali vikwazo ambavyo havina msingi,” msemaji wa Idara ya Biashara ya Marekani amesema.

Send this to a friend