China yaitoza Kenya faini TZS bilioni 25 kwa kutolipa mkopo wa SGR

0
35

China imeitoza nchi ya Kenya faini ya Ksh bilioni 1.31 [sawa na TZS bilioni 25.25] baada ya kuchelewesha malipo ya mkopo uliotolewa ili kujenga reli ya kisasa (SGR).

Kwa mujibu Business Daily, benki za China ziliipiga Kenya faini hiyo katika mwaka uliomalizika Juni Juni.

Kenya ilipokea zaidi ya bilioni 500 [sawa na zaidi ya TZS trilioni 9.6] kutoka kwa wakopeshaji wa China, wakiongozwa na Benki ya Export-Import ya China, kufadhili ujenzi wa SGR kutoka Mombasa hadi Naivasha.

Serikali yaombwa kupandisha gharama ya vipimo vya DNA

Kwa mujibu wa taarifa, walipakodi wamelazimika kulipa mikopo ya SGR kwa sababu mapato yanayotokana na huduma za abiria na mizigo kwenye reli hayatoshi kukidhi gharama za uendeshaji, ambazo takwimu zilionesha zilifikia Ksh bilioni 18.5 [sawa na TZS bilioni 356.8] dhidi ya mauzo ya Ksh bilioni 15 [sawa na TZS bilioni 289.3].

Kutokana na takwimu, SGR ilichapisha hasara ya Ksh bilioni 3.4 [sawa na TZS bilion 65.5], na ililipa Ksh bilioni 22.7 [sawa na TZS bilioni 437.8] katika ulipaji wa mkopo ambapo Kenya iliomba kuongezwa wa ulipaji wa deni kutoka kwa wakopeshaji wa pande mbili ikiwa ni pamoja na China, kwa miezi sita hadi Desemba 2021, ili kuiokoa kutokana na kutoa mabilioni kwa wakopeshaji wa Beijing, ombi ambalo lilipingwa hasa na Benki ya Exim ya China.

China inajumuisha moja ya tatu ya gharama zote za Kenya za kugharamia madeni ya nje kwa mwaka 2021/22.

Send this to a friend