Chuo cha Teknolojia cha India kuanzishwa nchini Tanzania
Serikali ya India inatarajia kuazisha Chuo cha Teknolojia (Indian Institute of Technology) nchini Tanzania ambacho kitakuwa kinatoa kozi ya masuala ya TEHAMA na kozi nyingine zinazoendana na mrengo huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kuongea na timu kutoka chuo hicho, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali ya Tanzania itashirikiana na nchi hiyo ili lengo la kuanzisha chuo hicho liweze kutimia.
“Wenzetu hawa wanataka kuanzisha Chuo hapa nchini tuliwaalika waje na tayari wamefanya mazungumzo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuahidiwa ardhi kwa ajili ya kuazisha huko, lakini kwa kuwa suala la elimu ya juu ni la muungano tunaangalia taratibu za urekebu kuona nini kinaweza kufanyika ili kazi hii iweze kuanza.
Aina 16 za vitabu zilizopigwa marufuku kutumika shuleni nchini
Wanataka kuanza kuchukua wanafunzi mwezi Oktoba mwaka huu ni muda mfupi sana kutokea sasa ila tutafanya kazi usiku na mchana kuona ni nini kinaweza kufanyika tukasonga mbele,” amesema.
Waziri Mkenda Amesema pia timu hiyo kutoka India imekwenda kutembelea Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela kilichoko jijini Arusha pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ili kuona vifaa vya kujifunzia na kufundishia vilivyopo na namna ambavyo wanaweza kufanya kazi kwa pamoja.