Chuo chawekwa chini ya uangalizi kwa kutoa programu iliyofutwa

0
38

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limekiweka katika uangalizi maalum kwa kipindi cha miaka mitatu Chuo cha DECCA Afya na Sayansi Shirikishi (DECOHAS) Dodoma kutokana na kukiuka taratibu za udahili.

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora NACTVET, Dkt. Jofrey Oleke amesema chuo hicho kimehusika na udahili wanafunzi 17 kwenye pogramu ya afya ya jamii ambayo ilifutwa mwaka 2019.

Aidha, amesema wanafunzi wote walioathiriwa tayari wamerudishiwa gharama zao zote na chuo kimewekwa kwenye uangalizi mkali.

Send this to a friend