Cleopa Msuya: Tusijisahau tukaelekea kwenye matatizo ya kisiasa

0
85

Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya amesema toka Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961 imeendelea kupiga hatua kubwa katika kuzingatia demokrasia hasa katika kuchagua viongozi wake bila kuwepo kwa mapigano tofauti na nchi nyingine.

Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha Dakika 45, amesema kutokana na hali hiyo, Tanzania inapaswa kuwa makini na kutojisahau ili kuepuka kuelekea kwenye matatizo ya kisiasa ambayo nchi za Afrika Maghagharibi zinapitia.

“Kwa kipimo hicho na kigezo hicho nafikiri tungesema Tanzania tuna bahati kwamba hata kama mtu atakosoa makosa yote, mambo yamekuwa mazuri, kitu cha kuchunga ni kwamba tusije tukajisahau tukaelekea kwenye matatizo ambayo nchi za West Afrika zinayo,” amesema.

Aidha, katika suala la katiba mpya amesema ni vizuri kama lingeangaliwa kwa kuzingatia ni kitu gani kimepungua katika katiba iliyopo na kuona jinsi ya kujadiliana na kupata muafaka ili yapitishwe na kuingizwa katika katiba iliyopo.

Lissu kushtakiwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo

Mbali na hayo, ameshauri Benki ya Dunia na Waziri wa Fedha wafanye utaratibu wa kuelimisha watu kuhusu hali ya kiuchumi iliyoikumba dunia uliosababishwa na vita vya Ukaraine na janga la UVIKO-19 ambao unaweza kusababisha misaada na wawekezaji kupungua, na viongozi watoe mwongozo wa jinsi ya kupambana na tatizo hilo endapo litazidi kupamba moto.

Send this to a friend