Corona: ATCL kutumia ndege zake kubeba mizigo

0
15

Katika kukabiliana na changamoto za kibiashara zinazosababishwa na mlipuko wa virusi vya corona, Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) inatarajia kuanza kutumia ndege zake za abiria kubeba mizigo.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema hatua hiyo inafuata baada ya ATCL kupata kibali cha kubeba mizigo kutoka kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na watengenezaji wa ndege.

Ameongeza kuwa usafirishaji wa mizigo ndio utakuwa njia kuu ya kuingiza mapato kufuatia kupungua kwa abiria na nchi nyingi kuzuia safari za ndege ikiwa ni mikakati ya kukabiliana na COVID-19.

Matindi amesema kuwa ndege zote tisa za kampuni hiyo zitatumika kubeba mizigo kulingana na ukubwa wa mzigo lakini pia na umbali.

Hata hivyo hakueleza kama watalazimika kufungua viti vya ndege hizo, au zitabeba mizigo zikiwa na viti.