Daktari mwandamizi kutoka Canada amewashauri watu kutobusiana na wavae barakoa wanapojamiiana ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona vinavyoendelea kuisumbua dunia.
Dkt. Theresa Tam amesema kuwa kujamiia kumekuwa na changamoto kubwa katika janga hilo, hivyo ni vyema watu wakahakikisha wanakuwa salama hata wawapo sirini.
“Afya ya kujamiiana ni sehemu muhimu ya afya yetu kwa ujumla. Hata hivyo, kujamiina kunaweza kuwa kugumu katika muda huu wa #COVID19…,” imeeleza taarifa yake, huku akifafanua zaidi kuwa wanaojamiina wanajiweka katika hatari wakifanya hivyo na mtu anayetoka nje ya nyumba zao.
Amesema kwa walr watakaoamua kujamiiana, basi wachukue hatua kadhaa kujiweka salama ikiwa ni pamoja na kuepuka kugusan nyuso zao au wote kuvaa barakoa (funika pua na mdomo).
“Ushahidi wa sasa unaonesha kuna uwezekano mdogo sana wa kuambukizwa corona kupitia maji maji yaliyopo kwenye sehemu za siri,” ameeleza daktari huyo.
Hadi Septemba 7, 2020 asubuhi (EAT) jumla ya visa 27,292, 585 vimerpotiwa duniani kote ambapo kati hivyo waliopona ni 19,377,268 na waliofariki ni 887,554.