Corona: Diamond kuzilipia kodi ya miezi mitatu familia 500

0
39

Nyota wa muziki nchini Tanzania, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz ametangaza mpango wake wa kuzilipia kodi kwa miezi mitatu familia 500, ikiwa ni sehemu ya msaada wake wakati taifa likikabiliana na virusi vya corona.

Diamond amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameeleza kuwa, licha ya kwamba na yeye ni mhanga katika janga la corona, lakini anaamini kwa kidogo chake anaweza kuwasaidia wengine ambao ni sehemu ya muziki wake.

Hata hivyo amesema kwamba Jumatatu ataweka bayana utaratibu utakaotumika kutumizi azma hiyo.

https://www.instagram.com/p/B_Z5p4aJPXW/
Send this to a friend