Corona: Diamond Platnumz apata hasara ya TZS 3.5 bilioni

0
50

Nyota wa muziki nchini Tanzania, Naseeb Abdul maarufu kwa jina la sanaa, Diamond Plattnumz amesema kuwa amepoteza shilingi 3.5 bilioni kutokana na matamasha yake ya muziki kusitishwa.

Akizungumza leo asubuhi Diamond amesema kuwa janga la corona limepelekea shows zake kusogezwa mbele, kufutwa huku nyingine zikisimamishwa ikiwa ni hatua ya kudhibitia maambukizi ya virusi hivyo kwa kuepuka mikusanyiko.

“Mahesabu ya haraka haraka tumepiga na uongozi, unaona kabisa shilingi bilioni 3.5 inapotea mbele ya macho yako,” amesema Diamond.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita waliwekeza zaidi pamoja na kutoa nyimbo kali ikiwa ni pamoja na Yope Remix iliyotamba dunia, Kanyaga, Inama, Jeje, uwekezaji ambao umefanya uhajitaji wake kuwa mkubwa zaidi.

“Mwenyenzi Mungu amenibariki mwaka huu nilikuwa na shows [matamasha] nyingi. Japo sikuwa nimepost tour [ziara] yangu ya Marekani, lakini nilikuwa na shows kama 20, Marekani pekee,” ameeleza nyota huyo huku akimalizia kuwa shows anazozifanya nje ya nchi ndizo zinazomuingizia kipato zaidi.

Send this to a friend