Corona: Hatua za kuchukua kwa wenye wafanyakazi wa ndani kujikinga na Covid-19

0
76

Katika kukabilina na maambukizi ya virusi vya corona, watu wengi hasa wenye wasaidizi wa kazi majumbani mwao wameonesha kuwa na wasiwasi wa namna ya kuishi nao na kuhakikisha familia yote inabaki salama.

Hofu kubwa imekuwa kwa wale ambao wasaidizi wao hawakai eneo la kazi, bali hulazimika kwenda na kurudi majumbani mara zote.

Kutokana na kuwa dalili za maambukizi ya virusi vya corona huchukua hadi siku 14 kuonekana, hivyo ni muhimu sana tahadhari zote kuchukuliwa.

Katika kuhakikisha wote wanakuwa salama, hatua kadhaa zinashauriwa kuzingatiwa ambazo ni pamoja na;

  1. Waelimishe wasaidizi/msadizi wako kuhusu ugonjwa wa corona ili achukue tahadhari hasa awapo nje ya nyumbani.
  2. Wanapokuja nyumbani watumie mlango uliopo karibu na sink la kunawa ili wanawe kabla hawajagusa chochote au kusalimiana na mtu mwingine.
  3. Weka alama mlangoni za kuwakumbusha wote wanaoingia kuwa, wavue viatu, wanawe mikono na kusafisha sink kwa sabuni, wasafishe vitu walivyonavyo kama funguo, simu, na pochi.
  4. Waoge na kubadili nguo walizokuwa wamevaa kisha zifuliwe.
  5. Wavae barakoa muda wote wa kazi ili kujikinga na kuwakinga wengine.
  6. Kuwe na umbali wa angalau mita 2 kati ya mtu na mtu. Kama haiwezekani, wanafamilia wote wavae barakoa.
  7. Wanawe mikono kwa sabuni na maji tiririka
  8. Safisha mara kwa mara maeneo yaliyoshikwa kama vile vitasa vya mlango, koki za bomba, swichi za taa, meza, angalau mara mbili kwa siku.
  9. Kusiwepo na safari za nje ya nyumba wakati wa kazi
  10. Kuwe na uhusiano mzuri utakaomuwezesha msaidizi kuripoti dalili zozote za ugonjwa.
  11. Kama kuna uwezekano, m/wapatie nafasi ya kuishi nyumbani kwako.

Elimu ni muhimu sana, kwani kwa kufanya hivyo wataendelea kuchukua tahadhari hata wanapokuwa nyumbani wenyewe au nje ya nyumbani.

Send this to a friend