Corona: Kenya kufungua shule mwaka 2021

0
32

Wizara ya Elimu nchini Kenya imetangaza kuwa shule za msingi na na sekondari zitafunguliwa mwaka 2021, kutokana na athari zilizosababishwa na janga la corona.

Wazir wa Elimu, Prof. George Magoha amesema mitihani ya kidato cha pili na darasa la nane iliyokuwa imepangwa kufanyika mwaka huu haitofanyika tena, kwa sababu serikali imebadili msimamo wa kuruhusu wanafunzi kurejea shule.

Serikali imeeleza kuwa imefikia uamuzi huo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na wadau wote wanaohusika na elimu.

Kuhusu elimu ya juu serikali imeeleza kuwa vyuo vitafunguliwa kwa awamu ili kuhakikisha kuwa wanafunzi na wakufunzi wote wanakuwa salama muda wote wa masomo na kwamba chuo chochote ambacho kitashindwa kufuata kanuni za afya kitafungwa.

Hadi sasa taifa hilo limeripoti jumla ya visa 8,067, ambapo kati ya hivyo watu 164 wamefariki na wengine 2,414 wamepona.

Send this to a friend