Corona: Picha za hoteli ya Diamond Platnumz aliyotoa iwe karantini

0
81

Mwanamuziki Diamond Platnumz ametoa hoteli yake jijini Dar es Salaam ili kutumiwa na serikali kuwaweka watu wenye maambukizi au wanaoshukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Corona: Diamond Platnumz apata hasara ya TZS 3.5 bilioni

Msanii huyo amesema hilo mapema leo asubuhi ikiwa ni mchango wake katika kuisaidia serikali kwenye vita dhidi ya homa ya mapafu (COVID-19).

Mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul amesema hoteli hiyo aliyoinunua ipo Mikocheni B, jijini Dar es Salaam na ina vyumba zaidi ya 30.

Corona: Diamond kuzilipia kodi ya miezi mitatu familia 500

Hapa chini ni picha sita za hoteli hiyo;

Licha ya hatua hiyo, serikali haijasema chochote kama itatumia jengo hilo ama la.

Katika hatua nyingine, mwanamuziki huyo amesema kuwa atazisaidia kaya 500 kulipa kodi ya nyumba kwa miezi mitatu, ikiwa ni mchango wake kwa mashabiki wake ambao wameathiriwa na janga la corona.