Corona: Rais wa Malawi atangaza siku 3 za kufunga na maombi

0
38

Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera ametangaza siku tatu za kufunga na maombi ya kitaifa kuanzia leo Julai 16, 2020 hadi Julai 18, 2020 kumuomba Mungu awaondolee janga la virusi vya corona pamoja na kuwaponya wale wote wanaoumwa.

Aidha, Rais huyo ambaye pia ni kiongozi wa kidini amewasahi wananchi kumuomba Mungu awape afya njema watoa huduma za afya ambao wamekuwa mstari wa mbele kukabiliana na janga hilo tangu liliporipotiwa nchini humo lakini pia awalinde wale wote ambao hawana maambukizi wasiyapate.

Rais Chakwera amewasihi wananchi kuungana naye katika kutoa shukrani Jumapili Julai 19 mwaka huu, kutokana na mambo mengi ambayo Mungu amewatendea kama taifa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Chakwera ambaye alikuwa kiongozi wa upinzani alichaguliwa kuwa Rais wa Malawi katika uchaguzi wa marudio uliofanyika Juni 23, mwaka kuu, baada ya Mahakama ya Katiba kubatilisha uchaguzi uliofanyika Mei 21, 2019 kutokana na kujawa na kasoro.

Send this to a friend