Corona: Tanzania yazuia ndege kutua nchini kwa kipindi kisichojulikana

0
35

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezuia ndege za abiria kutua nchini kuanzia Aprili 11 mwaka huu ikiwa ni hatua nyingine iliyochukuliwa na serikali kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha homa ya mapafu (COVID-19).

Kwa mujibu wa taarifa ya TCAA, safari zote za ndege zilizokuwa zimepangwa na zile ambazo hazikuwa zimepangwa zimezuia hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.

Licha ya zuio hilo, TCAA imebainisha kuwa ndege za mizigo zitaruhusiwa kuingia nchini, lakini wahudumu wa ndege hizo watawekwa karantini kwa gharama zao katika maeneo yaliyotengwa na serikali kwa kipindi chote watakachokuwa nchini.

Mpaka Aprili 13, Tanzania ilikuwa imeripoti visa 46 vya maambukizi ya virusi vya corona, vifo vitatu na wagonjwa saba wamepona.

Send this to a friend